Jinsi ya kufanya Matangazo ya Sponsored (Hatua 5 Rahisi)

Je, wewe ni mfanyabiashara ambaye unataka kuitangaza biashara yako online? Unatamani kutafuta wateja zaidi online? Leo utaenda kujifunza namna sahihi ya kufanya matangazo ya biashara katika mtandao wa Facebook na Instagram (sponsored ads)

Katika hatua 5 rahisi kufuatisha, utaenda kufahamu jinsi ya kufanya sponsored ads kuanzia mwanzo mpaka mwisho

Twende pamoja,

1.Tengeneza Business Page/Account

Hatua ya kwanza kabisa ni kuwa na Page ya Facebook ,pamoja na Account ya Instagram ya Biashara (switch to business profile)

Na uhakikishe kwamba katika account/page yako, unaweka taarifa zote muhimu za biashara yako kama namba ya simu/whatsapp, location ulipo pamoja na maelezo kuhusu bidhaa/huduma unazouza

2.Tengeneza Mastercard/Visa card ya Malipo

Ili uweze kulipia matangazo yako,inakupasa uwe na kadi yenye uwezo wa kufanya malipo online(Internet Banking).

Unaweza kutumia kadi za benki kama NMB,CRDB lakini inabidi ziwe zimewezeshwa (activated) kufanya malipo online.

Au njia rahisi ambayo wengi tunaitumia,ni kwa card za mitandao ya simu (Vodacom na Airtel),ambao wamerahisisha huduma hii na unaweza kutengeneza card ya kulipia online na ukaweka hela za matangazo kupitia  M-pesa au Airtel Money

Tengeneza card yako na ukariri/note pembeni taarifa muhimu kama Jina lako, Card number,Expiry date(MM/YY) na namba za siri (CVV).

3.Fanya Settings za Tangazo lako 

Ukishakua na kadi,nenda sasa kwenye post yako ambayo unataka kuitumia kama tangazo Facebook au Insta.

Kisha bonyeza button ya “Boost Post” ili kuanza mchakato wa kutangaza kwa kuseti vitu vifuatavyo katika tangazo lako:

Utafanya settings za LENGO la tangazo (GOAL), Je,unataka watu wakiona Tangazo lako wafanye nini?

Kuna visit profile (watembelee profile yako), Visit website (Watembelee link),More Messages (wakutumie message DM au whatsapp) nk

Kisha utaseti Target Audience (watu gani waone tangazo) kwa vitu kama interests,age,location,gender nk

THEN Bajeti yako ya tangazo Kwa siku (Kuanzia $1/day) na Duration (Yani Tangazo liruke kwa siku ngapi?)

Kisha endelea.

4.Weka Payment Details (Card details)

Utaona sehemu ya kuweka payment method,bonyeza hapo na ujaze taarifa za kadi yako uliyotengeneza (hakikisha ina hela pia kuanzia $1)

Kisha jaza taarifa nyingine kama currency (USD $) na Location/Timezone yako

Submit and save payment method.

5.Create Promotion (Tengeneza promotion)

Ukishaweka payment info (kadi yako ya malipo) na ikakubali,basi hatua inayofuata ni kubonyeza button ya “Create Promotion

Hapo umemaliza,na tangazo lako utaona limeandiKwa Pending Approval.

Tangazo lako linakuwa limeenda katika review process ,ambapo linakaguliwa kama limekidhi vigezo na masharti ya kutangaza ya (Facebook Ads policy), then litakuwa Approved.

Process hiyo mara nyingi hukamilika ndani ya masaa 24 au chini ya hapo, then tangazo lako litaanza kuruka.

HONGERA SANA,

Ukifuatisha hatua hizo vizuri,utakuwa umeweza kufanya tangazo lako la kwanza la sponsored.

Kinachobaki sasa kwako kama mfanyabiashara ni kujiongeza, fanya matangazo kadhaa,

angalia performance yake inaendaje,unapata wateja?Je, Kuna sehemu unakwama?

Endelea kujifunza namna ya kuboresha matangazo yako, na kama Unahitaji msaada zaidi au muongozo, usisite kuwasiliana nasi (MATANGAZO ACADEMY)

Jiunge na wafanyabiashara wenzio wanaojifunza Bure katika magroup yetu ya whatsapp.

Kama una swali lolote kuhusu Sponsored ads, karibu uulize katika comments apo.

Endelea kufuatilia blog yetu pia kwa mada kama hizi kila wiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published.