Swali ambalo huwa naulizwa sana na watu ambao wanataka kuanza kufanya Matangazo ya Sponsored ni hili
“Gharama zake zipoje?”
Na hapa wengi huwa wanatamani Kufahamu watumie bajeti ya kiasi gani, ili waweze kupata matokeo mazuri.
Leo nitaenda kujibu swali hili na nitakupatia muongozo kama ifuatavyo:
1. Bajeti ya Kuanzia
Unaweza kuanza Sponsored Ads na bajeti ya Dola moja kwa siku, yaani $1/day (Haizidi Tsh. 2400/= kwa siku)
Na unaweza kurusha tangazo kwa siku moja au zaidi.
Hivyo bajeti yako ya siku utazidisha na idadi ya siku utakazorusha Tangazo.
Mfano $1/day x 5 days = $5
2. Bajeti ya Kupata Matokeo Mazuri
Hapa cheza na kuanzia $3,$5,$10+ per day.. Kulingana na mfuko wako Unasemaje.
Hii itakusaidia Tangazo lako kuonekana kwa watu wengi zaidi, kuliko ukiweka $1/day.
Na utaweza kuIscale Biashara yako kuanzia hapa.
In Conclusion:
Anza na BAJETI ya kawaida uone performance ya Tangazo lako inakuwaje,
Kisha Ongeza bajeti Taratibu kulingana na Matokeo unayopata katika Tangazo lako
Ukiongeza haraka haraka watakula hela yako haraka haraka bila kukupatia Matokeo mazuri
Niambie katika comment hapo,wewe huwa unaweka bajeti kiasi gani katika matangazo yako?
Endelea kujifunza zaidi kuhusu Sponsored Ads, na kama Unahitaji msaada zaidi au muongozo, usisite kuwasiliana nasi (MATANGAZO ACADEMY)
Jiunge na wafanyabiashara wenzio wanaojifunza Bure katika magroup yetu ya Whatsapp.
Na Kama una swali lolote kuhusu Sponsored Ads, karibu uulize katika comments apo.
Endelea kufuatilia blog yetu pia kwa mada kama hizi kila wiki.