Kama unafanya biashara…bila shaka unatafuta wateja. Kuna njia nyingi za kupata wateja,na mojawapo ni kwa kufanya matangazo ya mtandaoni maarufu kama Sponsored ads.
Ukiwauliza wafanyabiashara wengi wanaofanya sponsored,wanafanya wakiwa na lengo kuu la kutafuta wateja na kuuza bidhaa/huduma zao.
Ni mtazamo ambao uko sawa,lakini kuna vitu vya ziada ambavyo unaweza kupata pia kama faida ya kufanya sponsored, ukiacha wateja.
Na leo nitaenda kukuonesha faida 5 nyingine ambazo utazipata katika biashara yako, kama ukianza kufanya sponsored leo hii.
Na kama wewe unafanya matangazo tayari,angalia ni kwa namna gani unaweza kubadilisha approach yako ya matangazo (usifocus na kuuza kila saa),ili uweze kupata faida hizi pia
1.Kutengeneza/Kuongeza Business awareness
Faida ya kwanza ya matangazo ya sponsored, ni kutengeneza business awareness kwa wateja wako watarajiwa.
Unapoitangaza biashara yako,unaongeza wigo wa kufahamika sokoni, kwamba flani anauza kitu flani na anapatikana sehemu fulani
Kumbuka matangazo yako yanaonekana kwa watu wengi,hivyo kila unavyozidi kuonekana, ndivyo itakusaidia siku yule mtu ambaye amekuona ukijitangaza akihitaji kitu unachouza.
Inakuwa rahisi kukutafuta wewe, kwa sababu tayari anakujua na anafahamu unakopatikana.
Achana na wafanyabiashara wanaofocus kuuza tu katika kila tangazo wanalofanya, Wewe tenga kiasi flani cha bajeti yako ya matangazo, kufanya hizi campaigns za awareness (utanishukuru baadae)
2.Kuelimisha Wateja kuhusu Bidhaa/Huduma yako
Kama umeshafanya marketing ya biashara yako online, utakuwa umeshakutana na maswali ya wateja.
Na hapa inategemea sana biashara yako unayofanya….
Ila kwa watu wanaouza bidhaa mbalimbali mfano bidhaa za afya,tiba lishe,urembo au wanaotoa huduma kama kusajili Makampuni, Graphic Designers, Insurance, Watu wa IT nk
Kabla ya kuuza kwa mteja,lazima tu kuna maswali atakuuliza, na inabidi umjibu na umweleweshe ndio anaweza kununua ,(la sivyo utampoteza).
Sasa utajibu watu wangapi kila siku? Na ukizingatia wengi wanauliza maswali yale yale, ambayo jana na juzi umetoka kujibu watu wengine.
Solution? Tumia matangazo yako kama sehemu ya kutoa Elimu kwa wateja wako, na jitahidi ujibu yale maswali yao ambayo ni common.
Na hii itakusaidia ukija kuwauzia,inakuwa rahisi sana…jaribu uone.
3.Gharama zake ni nafuu
Faida nyingine ya kutumia matangazo ya sponsored inakuja katika unafuu wake wa gharama, ukilinganisha na njia nyingine kama matangazo ya radio/TV au kuweka Mabango (Billboards)
Una uwezo wa kuanza sponsored na $1 tu kwa siku,( ambayo haizidi hata 2400),wakati ukitaka kutangaza redioni au TV inakubidi ujipange vizuri kwanza.
Ukiwa na bajeti yako kuanzia elfu 30,50 na kuendelea,unaweza kufanya sponsored na ukaanza kuona matokeo vizuri tu, na hii inawafaa sana wafanyabiashara wadogo ambao ndio wanaanza kujitangaza ili kukuza biashara zao
Jitangaze,uza,wekeza zaidi katika matangazo,uza zaidi na mwisho ikuze biashara yako na mtaji wako.
4.Unaweza kulenga Watu Specific waone Tangazo lako
Siri ya kwanza ya kuuza kupitia matangazo,ni kuhakikisha matangazo yako yanaonekana na watu sahihi (Target audience)
Kumbuka sio kila mtu ni mteja wako,na ukitaka uhangaike kuuza,jaribu kumuuzia kila mtu.
Faida ya kutumia sponsored ads, ni uwezo wa kuchagua ni watu gani waone tangazo lako,na sio kila mtu.
Una uwezo wa kutengeneza Audience yako kwa kuchagua location waliyopo (mikoa,wilaya,sehemu), Interests zao, Umri(miaka 18-65+), pamoja naJinsia (wanaume au wanawake au wote) na kisha ukawaonesha hao tu matangazo yako
Ukijfunza kutengeneza audience sahihi,utaona matangazo yako yanavyoperform vizuri.
5.Kutangaza Special offers/New offers
Njia mojawapo ya kuboost mauzo yako ni kutoa OFA mbalimbali kwa wateja wako.
Let’s say una mzigo mpya umeingia, au unamzigo umekaa unataka kuutoa chap chap, au katika huduma yako kuna discount umeamua kutoa kwa muda fulani
Ukitumia sponsored ads, na ukawaeleza vizuri wateja wako sababu ya kutoa ofa hizo,unaweza kushangaa jinsi utakavyopata wateja wa kutosha.
Cha kuzingatia hapa ni wewe kuwa mkweli, na usiwe mtu wa kutangaza OFA OFA kila siku, watu watakuchoka na hawatakutilia maanani tena hata siku ukiwa serious.
In Summary
Wewe kama mfanyabiashara yakupasa ujiongeze, na uwe wa tofauti sokoni ili iuweze kuvutia wateja zaidi.
Ukiona wenzio wote wanahangaika na sponsored,wakipush matangazo ya kuuza kila saa (Buy this,Buy now),
Tumia hiyo kama fursa ya kufanya matangazo yako kiutofauti (add value to your clients first,then sell)
Tumia ideas ulizopata hapo juu katika matangazo yako,kisha changanya na matangazo ya kuuza kawaida,matokeo yako yataongea.
Endelea kujifunza namna ya kuboresha matangazo yako, na kama Unahitaji msaada zaidi au muongozo, usisite kuwasiliana nasi (MATANGAZO ACADEMY)
Jiunge na wafanyabiashara wenzio wanaojifunza Bure katika magroup yetu ya whatsapp.
Na Kama una swali lolote kuhusu Sponsored Ads, karibu uulize katika comments apo.
Endelea kufuatilia blog yetu pia kwa mada kama hizi kila wiki.