Tunaendelea na Mada yetu ya Social Media Marketing, na Leo tutaenda kugusia suala zima la Content.
Social Media accounts zinaendeshwa na Content,hivyo inakubidi uposti kwanza ndio uweze kuuza
Leo Utaenda kufahamu Aina 3 muhimu zaidi za contents, na ni namna gani uzitumie katika kufanya Marketing ya Biashara yako mtandaoni,
Utaenda kufahamu ni Makosa gani uepuke kuyafanya katika kila aina ya content
Hivyo,soma huku ukiangalia Account yako ilivyo sasa na Contents unazoposti
Ili uweze kufahamu nini na nini unaweza kurekebisha na kuboresha zaidi
Twende pamoja
Aina 3 za contents na Jinsi ya kuzitumia Vizuri
1. IMAGES (Picha)
Hapa kwa wengi wanafanya vizuri,hivyo basi sitatumia muda mrefu kupaelezea, lakini zingatia hivi:
Hakikisha Quality ya picha zako ni nzuri na ya kuvutia, Kwani Picha nzuri za bidhaa zinashawishi watu kununua zaidi
Na zinakuonesha kuwa wewe Mfanyabiashara uko serious na kitu unachokifanya,
So usiposti picha ilimradi umeposti, bali jitahidi iwe katika best quality possible
Mtu akiingia tu kwenye account yako,picha zako ziwe zinamvutia na kumshawishi.
2.VIDEOS
Tafiti zinaonesha Video contents zinapata Engagement (Likes,Comments) zaidi kuliko Picha.
Na Kusema ukweli Video zinatembea sana siku hizi, kuliko hata Picha
Ndio maana ukiingia Instagram, utaona ukiscroll kidogo tu unakutana na videos za kutosha
Instagram Reels, Tiktok Videos na Youtube Shorts zinaongeza idadi ya watu wanaopenda kuangalia videos fupi fupi (short form content) kila siku
Hivyo basi, kama Attention ya watu ipo huko…wewe kama mfanyabiashara hupaswi kubaki nyuma, jitahidi na wewe utumie fursa hiyo kuonekana
Mimi nilishawahi kupata Mteja wa website kutoka India,sababu ya Instagram Reels,….Niliposti,akaiona..akanicheki DM, tukafanya nae kazi.
Tumia Videos kuonesha Biashara yako,Bidhaa/huduma zako na kujionesha wewe pia ili watu wakufahamu na kukuamini.
Muhimu zaidi, Zingatia Quality katika Videos,Simu yako inatosha kuanzia lakini hakikisha unaporecord video..mwanga uwepo wa kutosha.
Na kama hujaanza kutumia videos kabisa, ANZA LEO
3.TEXT BASED POSTS
Hii ni aina nyingine ya content ambayo unaweza kuitumia, Mahususi kabisa kwa ajili ya kuelimisha wateja kuhusu Bidhaa/huduma yako
Mfano; unauza dawa za Tiba lishe(supplements), unaweza kuwa na posts kadhaa zenye maelezo kwa watu mfano dalili za ugonjwa fulani,changamoto na jinsi ya kutibu
Hizi zinamsaidia mteja wako aweze kupata taarifa zote muhimu anazohitaji ili afanye maamuzi ya kukutafuta au lah.
Changamoto ambayo nimeiona kwa watu wengi, ni kwamba wanacopy na kutumia posts zile zile zinazofanana, na nyingine ziko poorly designed, maneno mengi,rangi hazivutii kabisa hata kusoma
Jitahidi unapotumia Text based posts, ziwe zinaweza kusomeka vizuri,design iwe nzuri na muhimu zaidi ziwe Branded kulingana na biashara yako
Kama una lengo la kujenga Brand, basi hakikisha unazingatia Branding tangu mwanzo mpaka mwisho.
In Conclusion
Mfanyabiashara aliye serious na kufanya Biashara Mtandaoni, Lazima atazingatia suala zima la Ubora katika Contents zake anazoposti.
Ili kuhakikisha anajiongezea nafasi ya kuvutia wateja wapya kila siku, na kupata matokeomazuri anapofanya matangazo yake (Sponsored)
Je, unataka kufahamu ni aina ipi exactly ya Content zinapendwa na Wateja, Contents zipi zitakuongezea Engagement? Na Zipi zitakuletea Mauzo zaidi?
Endelea kufuatilia mada zijazo,tutagusia kiundani suala hilo
kama una changamoto na unahitaji Msaada Binafsi,ili uweze kufanya Matangazo yako vizuri,
Bonyeza hapa Kuja whatsapp moja kwa moja,nitakuskiliza