Introduction to Digital Marketing 2022 (In swahili)

DIGITAL MARKETING ni nini? Je, ina umuhimu gani kwako wewe kama Mfanyabiashara wa Dunia ya leo?

Leo Tutaenda kugusia 

  1. Maana ya Digital Marketing
  2. Utofauti wake na Traditional Marketing
  3. Jinsi ya Kutumia Fursa hii katika Biashara yako

Twende pamoja,

Digital Marketing kwa lugha nyepesi kabisa ni kitendo cha kufanya Marketing na kuitangaza Biashara yako kwa kutumia Digital channels (Online Mediums)

Unaweza kuiita Online Marketing pia,

Digital marketing inahusisha mchakato wa kutangaza na kufikia wateja wako kwa kutumia Online channels kama vile Social media, Website,Email,Search Engine kama Google,Youtube nk…

Kwa hiyo unapotumia njia hizo,tayari tunasema unafanya Digital Marketing

Watu wengi tumezaliwa na kukua na zile Traditional ways of Marketing kama vile Matangazo ya Radio, TV, Magazeti,na Billboards, Mabango,Vipeperushi,Business cards,nk

Lakini Mambo yamebadilika , kuanzia mwaka 2015 kwenda mbele,hapa kwetu Watu walianza Kuchangamkia Fursa hii ya Digital Marketing.

Sasa hivi wala huhitaji kwenda katika Radios na TV ili kuanza kutangaza biashara yako, 

Unaweza ukaanza kutangaza biashara yako hapo hapo ulipo, Kwa kutumia  simu yako, na ukapata Wateja vizuri kabisa.

Na uzuri wa Digital Marketing,wala huhitaji kuwa na bajeti kubwa ya Matangazo ili uanze kutangaza Biashara yako,unaweza Kuanza hata na Dola moja ($1) tu kwa siku.

Siku hizi Watu wengi wanafanya Matangazo, ndo maana ukipita Insta au Facebook,unakutana na Matangazo kibao (Sponsored Ads)

Watu wanachangamkia fursa,.. fursa ya kuonesha biashara zao machoni mwa wateja watarajiwa.

What about you??

Je, wewe unatumia fursa hii kuiweka biashara yako ionekane machoni pa watu wengi kila siku?

Au bado umejificha,unafanya Marketing kizamani na unalalamika hupati wateja?

Nikuibie siri 2 hapa za chap chap,kisha tufunge mada kwa leo

  1. Mitandao inatumiwa na watu wengi sana, Hivyo kama unauza Bidhaa/Huduma bora ambayo unaamini kabisa ina thamani (Value) kwa watu,ni wajibu wako kuhakikisha unaiuza kwa watu hawa kwani unawasaidia pia
  1. Digital marketing sio lelemama,usidhani ni kuweka Matangazo tu na kusubriri Mvua ya wateja,nope..…lazima ujipange,uwe na strategy na uzingatie vitu mbalimbali kama Targeting,offer,CTA,objectives,copy,budget nk ambavyo ndio vitakuletea matokeo katika matangazo yako

Hivyo basi,kama wewe ni mfanyabiashara na ungependa kutumia fursa hii ya Digital Marketing, au tayari umejaribu kufanya Matangazo, lakini hujapata matokeo mazuri,….unaona unahitaji Msaada

I have good news for you,

Usihangaike peke yako Tena,Tumeanzisha platform hii ya MATANGAZO ACADEMY kwa ajili yako.

Tunashea Knowledge na Tips mbalimbali za Social Media marketing, Sponsored Ads na Business kwa Ujumla (Kutangaza na Kuuza online).

Unaweza kujifunza katika Blog yetu hapa, Na GROUP la whatsapp la FREE Training ambako tunatoa mafunzo kila wiki.

Na kama unahitaji Practical help, ili uanze kufanya matangazo yako vizuri,tutakuhudumia pia.

Bonyeza hapa  Kuja whatsapp moja kwa moja.

Ahsante kwa kufuatilia Article hii mpaka mwisho, kama una swali lolote usisite kuuliza hapa chini..Nitakujibu

Usisahau kushea article hii na mwenzio ajifunze pia, tukutane next post

Leave a Reply

Your email address will not be published.